Mfahamu Mmiliki wa Wasafi TV ambaye ndiye Muandaaji wa Tamasha la Fiesta


Ni miezi kadhaa sasa imepita tangu kituo kipya cha runinga cha Wasafi TV kianze kurusha matangazo yake hewani, huku kukiwa na mkanganyiko mkubwa kwenye jamii juu ya mmiliki mkubwa wa kituo hicho.


Diamond Platnumz katikati kwenye picha
Sintofahamu ya mmiliki hasa wa kituo hicho, ilikuja baada ya baadhi ya watu kudai kuwa mmiliki ni Diamond Platnumz wengine wakidai kuwa mmiliki ni Joseph Kusaga, ambaye ni Ofisa Mtedaji wa Clouds Media Group.

Swali ni Je, ni nani haswa mmiliki wa Wasafi TV?

Kwa mujibu wa mtandao wa gazeti la Mwananchi, umeeleza kuwa Wasafi TV inamilikiwa na watu watatu, ambapo kati ya watu hao jina la Joseph Kusaga halipo.<img src="https://www.ghettoradio.co.ke/wp-content/uploads/2018/08/wasafi-tv.jpg" alt="Related image"
Majina hayo ni Juhayna Zaghalulu Ajmy ambaye ndiye anamiliki hisa nyingi kwa asilimia 53 ya Wasafi TV, akifuatiwa na Nasibu Abdul Juma, a.k.a Diamond Platnumz, anamiliki asilimia 45 na Ali Khatib Dai anamiliki asilimia mbili.

Unaweza ukajiuliza huyu Juhayna Zaghalulu Ajmy ambaye anamiliki asilimia nyingi za Wasafi TV ni nani?





Juhayna na mumewe Joseph Kusaga
Huyu ni mke wa Joseph Kusaga ambaye pia ndiye C.E.O wa Kampuni Prime Time Promotions ambayo ndiyo iliyoanzisha na kuendesha tamasha la Fiesta kwa zaidi ya miaka 10.




Ujio wa Wasafi TV ambayo ipo chini ya Kampuni ya Wasafi, umekuwa mwiba zaidi kwa Kampuni ya Clouds Media Group ambayo inamiliki Clouds FM na Clouds TV.



Kampuni ya Clouds Media inajishughulisha zaidi na biashara ya burudani, kupitia tamasha la Fiesta ambalo lipo chini ya Primetime Promotions, kusimamia wanamuziki na studio za kurekodi muziki kupitia THT.

Kwa upande mwingine, Kampuni ya Wasafi pia nayo inamiliki lebo ya muziki ya WCB, Studio za kurekodia muziki Wasafi Records, Vyombo vya habari kama Wasafi FM & Wasafi TV, platform za kusambaza nyimbo mtandaoni Wasafidotcom na pia kampuni hiyo ndio waandaaji wa tamasha la Wasafi Festival.

Mzozo uliopo kati ya Media hizo, unaonekana kupuuzwa na baadhi ya watu, hii ni kutokana na ukaribu mkubwa uliopo kati ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa Clouds Media, Joseph Kusaga na C.E.O wa Wasafi, Diamond Platnumz.

Ukaribu wa Diamond na Kusaga, ndio uliopelekea watu wengi kuhisi kuwa huenda DJ huyo wa zamani ana hisa zake ndani ya Wasafi TV. Mpaka sasa Clouds FM na Clouds TV hawapigi nyimbo za wasanii wote wa WCB, jambo ambalo linazidi kuchochea uhasama.